Shule iliyoshika nafasi ya mwisho matokeo darasa la saba yapewa bendera nyeusi


Na. Baraka Messa, Mbozi

Shule  yapeperusha bendera nyeusi kutokana na kushika nafasi ya mwisho kimkoa katika matokeo ya darasa la saba ya mwaka 2018, wilayani mbozi mkoani Songwe ikiwa ni onyo na fundisho kwa walimu na viongozi wa kijiji na kata katika eneo hilo kutokana na kushika nafasi ya mwisho kiwilaya na kimkoa.

Shule ya Msingi Namlonga iliyopo kijiji cha Namlonga kata ya Manyara takribani kiliomita 45 kutoka makao makuu ya mkoa wa Songwe  matokeo ya darasa la saba msimu wa 2018 ilishika nafasi ya mwisho kimkoa kati ya shule 420  na  nafasi ya mwisho kiwilaya kati ya shule 161.

Mkuu wa shule hiyo Hassani Mlilo alisema walipewa bendera hiyo waipeperushe na viongozi wa Halmashauri ya Mbozi kama fundisho kwa walimu na viongozi wa kijiji na kata kutokana na matokeo hayo mabaya ambayo hayajawahi ikumba shule hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1991.

Alisema sababu zilizoifanya shule hiyo kushika nafasi ya mwisho katika orodha ya shule zote wilayani Mbozi na mkoani songwe kuwa ni pamoja na ushirikiano mbaya wa wazazi kwa walimu kuanzia kwa wanafunzi wa elimu ya awali mpaka darasa la saba, wanafunzi kutembea umbali mrefu na  miundo mbinu ya madarasa na vyoo kuwa mibovu hali iliyopelekea mwalimu Mkuu kutumia muda mwingi katika kusimamia miundo mbinu hiyo baada ya fedha za serikali za kuboresha miundo mbinu shuleni hapo kuingia mwakajana .

"Shule yetu ilishika nafasi ya mwisho katika orodha ya shule zote kimkoa na kiwilaya na kimkoa kwa kupata wastani wa asilimia 28 , matokeo ya mwakajuzi tulikuwa na ufaulu wa asilimia 70 lakini kutokana na kutingwa zaidi na uboreshaji miundo mbinu shuleni hapa ili changia sisi walimu kushindwa kusimamia vizuri taaluma" alisema Mlilo.

Mlilo alisema wameamua kujipanga ili kutoa bendera nyeusi ambayo wameipata kutokana na matokeo mabaya kwa kuboresha miundo mbinu ya vyoo ambayo ilikuwa kero kwa wanafunzi, kufundisha muda wa ziada , kuweka kambi wanafunzi ili kuwasimamia nyakati za usiku kuwafundisha na kujisomea.

Aliitaja sababu nyingine ambayo ni mpango wa muda mrefu kuwa ni kuboresha elimu ya awali kwa kuwaandalia vizuri watoto hao mazingira mazuri ya kujifunzia pamoja na vifaa vya kufundishia ambapo tayari wana mwalimu aliyepata mafunzo ya ufundishaji elimu hiyo.

"Tumegundua kuwa misingi mibovu kwa wanafunzi pia hupelekea watoto kuto fanya vizur matokeo darasa la saba, hivyo tumeamua kuweka nguvu kwa watoto wa awali kwa kuwatengea darasa lao na kuwa na mwalimu maalum kwa ajili yao ili waandaliwe wakiwa wadogo kupenda shule" aliongeza Mlilo.

Meshack Gunza Mwenyekiti wa kijiji hicho alipohojiwa kuhusiana shule yao kupeperusha bendera nyeus alisema kuwa ushirikiano mbaya kati ya wazazi na walimu ndio chanzo cha shule hiyo kupata bendera hiyo nyeu ambayo wanaiona kama msiba.

Alisema wameandaa mikakati ya kuhakikisha bendera hiyo inatoka shuleni hapo kwa kuunganisha nguvu na kutoa ushirikiano mzuri kwa walimu na kuwafuatilia vizuri watoto wao , huku wakichukuliana hatua za kinidhamu kwa kulipishana faini kwa wazazi wanaokwamisha watoto kwenda shuleni .

"Saizi tunashirikiana vizuri na walimu wetu nane (8) tumekamilisha madarasa , matundu ya vyoo na tayari tumeandaa darasa kwa ajili ya watoto wanaosoma elimu ya awali ili kuwajengea watoto wetu tabia ya kupenda shule mapema, hii itatusaidia kutopata matokeo mabaya kama ya msimu uliopita" alisema mwenyekiti.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi, Elick Minga alisema shule hiyo ilipewa bendera ikiwa ni ishara ya ya kuitaka ifanye juhudi ambazo zitapelekea kufanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba wa mwaka huu 2019.

alisema kuwa wamekuwa na utaratibu wa kutoa bendera nyeusi kwa shule zinafanya vibaya matokeo ya darasa la saba na kata zinazofanya vibaya  lengo kubwa likiwa ni kuongeza juhudi kutokana na aibu ya bendera nyeus ambayo ni ishara ya kuonyesha kuwa umefel kwasabu huwekwa shuleni ili kila mtu aone .

"Tuna imani shule hii itatoka huko iliko na kufanya vizuri katika msimu huu ili iweze kutoa bendera hiyo ambayo ni aibu kwa walimu na viongozi wa vijiji na kata wanaotoka iliko shule hiyo" alisema Minga .

 Frenk Samson mratibu wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto nchini (Early Childhood Development -ECD) alisema ili mtoto apende shule na aweze kufanya vizuri mitihani yake, jamii inatakiwa kubadilika kwa kuwekeza kwa mtoto tangia mdogo kwa kuwapeleka katika shule za awali .

alisema mtoto akisoma vizuri awali anakuwa na utayari wa kujifunza pindi anapoingia darasa la kwanza kwa kuwa huwa tayari amezoea kucheza michezo na shughuli za kimaarifa kwa maana ya kumwandaa kusoma, kuandika kuhesabu na kujieleza ambako huboresha matokeo anapohitimu elimu ya msingi.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items