Takriban watu 54 wamefariki na wengine 194,000 wameathiriwa na mvua kubwa ambayo imesababisha mafuriko kote nchini Sudan.
Msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA), Geneva Jens Laerke alisema kuwa vifo hivyo vilisababishwa hasa na maporomoko ardhi, kuvunjika kwa nyumba na hitilafu za umeme.
"Zaidi ya nyumba 37,000 zimeharibiwa huku msimu huo wa mvua ukitarajiwa kudumu hadi Oktoba na shirika linahofu kuwa kutakuwa na ongezeko la mafuriko," msemaji huyo alisema.
