Loading...

8/19/2019

Harmonize azungumza alichoambiwa Ikulu Dar


Msanii wa muziki kutoka Label ya WCB, Harmonize akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Jakaya Kikwete wakinena jambo walivyokutana Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Harmonize, alipata mualiko wa kuhudhuria dhifa maalum iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa heshima ya viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika ya Kusini (SADC).

"Nilipata Nafasi Ya Kujumuika Katika Dhifa Ya Taifa Ilioandilia Na Raisi Wetu Kipenzi Doctor John Pombe Magufuli statehouse Jijini Dar es salaam Naamini Nilikuwa Pale Kuwakilisha Vijana Wengi Walio Mtaani Na Wenye Ndoto...!!! 🙏🙏 Hakika ilikuwa Bahati Kwangu Kukutana Na Viongozi Wa Ngazi Za Juu Kabisa Kila Nilie kutana Nae Pale Ndani Alinipongeza Sana..!! Na Kuniambia wanajivunia Uwepo Wangu Katika Hili Taifa Tukufu Ilinipa Moyo Na Somo La Kwamba Kupitia Kipaji Chako Au Kazi Yako Hiyo Hiyo ifanye Kwabidi...!!! Utatimiza Kila Aina Ya Ndoto Yako...!!! Na Kupewa Kila Aina Ya Heshima..!! Kijana Mwenzangu Chukua Hiyo ."

"Lakini Mwishoni Kabisa Nikakutana Na Swahiba former President D.R Jakaya Mrisho Kikwete Tulifurahi Sanaa Akaniambia Wewe Sasahivi Sio Msani Tena Wewe Ni Mwanamuziki Ni Wakati Wa Kuifanya Tanzania Iendele Kuwa proud Na Wewe Watanzania Woteeee Wanakupenda Na Wana kusupport Go go go.....!!! Nami Nikamwambia Sitoweza Kuwaangusha Na Sitoweza kuku Disappoint Yani Subiri Tuu Uone Hili Movie Linavyoenda...!!! Akacheka Sana mwisho Akaniambia Mimi Nakutakia Kila La Heri...!!! Love You Dady."

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger