Mawakala wa Mesut Ozil sasa kutua nchini Marekani, kisa?


Vinara wa kikosi cha DC United nchini Marekani wamemtaka kiungo Mesut Ozil kukubali mshahara mdogo ili ajiunge na miamba hao wa Major League Soccer (MLS) wanaopania kulijaza pengo la Wayne Rooney.

Ozil kwa sasa ndiye mchezaji wa pili baada ya Alexis Sanchez wa Manchester United anayepokea mshahara wa juu zaidi katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

 Nyota huyu wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani kwa sasa hupokea Sh46 milioni kwa wiki. Sababu ya DC United kumtaka Ozil ni kujaza nafasi ya Rooney ambaye kwa sasa anajiandaa kuanza majukumu ya kuwa kocha na mchezaji wa Derby County mnamo Januari 2020.