Loading...

8/15/2019

Mbunge Viti Maalum CCM atoa vifaa vya ujenzi


Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Amina Mollel ametoa vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya Saruji 150 pamoja na bati 48 ili kusaidia ujenzi wa miundombinu ya shule katika halmashauri ya Arusha DC wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Mollel amekabidhi mabati 38 pamoja na mifuko 30 ya sementi Shule ya Sekondari Olemedeye katika Kata ya Nduruma pia amekabidhi jumla ya mifuko 50.

Aidha katika Shule ya Msingi Losinoni iliyopo katika Kata ya Oldonyowas amekabidhi mifuko 20 kwa ajili ya ujenzi wa Choo cha Waalimu. Shule ya Msingi Mringa pia amekabidhi mifuko 25 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya kujistiri watoto wa Kike wanapokuwa kwenye hedhi.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger