Mshambuliaji wa Mamelodi Sundowns Habib Kyombo afanyiwa upasuaji wa goti


Mshambuliaji wa Mamelodi Sundowns ya nchini Afrika Kusini Habib Kyombo amefanyiwa upasuaji wa goti mara baada ya kuumia akiwa mazoezini.

Baada ya kufanyiwa vipimo iligundulika kwamba hayakuwa maumivu mapya bali alijitonesha jeraha alilolipata siku za nyuma akiwa anaichezea Singida United.

Ili mchezaji huyu kuweza kupona iliamuliwa afanyiwe upasuaji ambao utamlazimisha kuwa nje ya uwanja kwa miezi isiyopungua minne.