Rais wa Marekani Donald Trump amesema alilazimika kuikabili China kuhusu biashara hata kama ilisababisha athari ya muda mfupi katika uchumi wa Marekani kwa sababu China imekuwa ikifanya udanganyifu kwa Marekani kwa miongo mingi.
Matamshi hayo mazito ya Trump yamekuja saa chache kabla ya serikali yake kutangaza idhini ya mauzo ya ndege za kivita aina ya Lockheed Martin F-16 kwa Taiwan, hatua ambayo kwa hakika itaikasirisha China na kuuwa kabisa uwezekano wa kupatikana makubaliano ya haraka ya kibiashara.
Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence pia ameichokoza China kuhusu mada nyingine tete, Hong Kong, akiitaka serikali ya Beijing kuheshimu uadilifu wa sheria za mkoa huo ambao ni koloni la zamani la Uingereza, katika namna inavyoyashughulikia maandamano jijini humo.