Tembo aliyekonda kupitiliza agusa hisia za wengi


Picha za kusikitisha za tembo zimeibua gumzo mitandaoni baada ya kuonekana akiwa amedhoofu mwili huku mbavu zake zikionekana.

Tembo huyo wa kike aitwaye ‘Tikiiri’ mwenye umri wa miaka 70, alionekana katika Tamasha la Perahera huko Sri Lanka mwaka huu akiwa na tembo wengine 60, licha ya mwili wake kuwa dhaifu na kuonekana mgonjwa.

Tamasha hilo au Sikukuu ya kabila la Wabudhi ambayo inafanyika kwa siku kumi nchini humo inawatumia wanyama waliopambwa kama tembo, pamoja na mamia ya waigizaji wakiwemo wachezaji wa densi, wachezeaji moto na wanamuziki.

Picha za tembo huyo zilirushwa mtandaoni na shirika la Save Elephant Foundation kuashiria Siku ya Tembo Duniani. Wakati Tikiiri akionekana kupendeza kwa watazamaji wa sherehe hiyo baada ya kuvikwa mavazi yake mwili mzima, hakuna mtu anayeona mwili wake au hali yake dhaifu, kwa sababu ya mavazi yake.

Mpya zaidi Nzee zaidi