Usajili wa ndoa Tanzania: sio sheria ya Makonda



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania, Paul Makonda mpango wa kuweka hadharani ndoa zilizosajiliwa katika mkoa huo liliibuka kutoka kwa wananchi wenyewe wakieleza changamoto zinazowakabili, na 'sio sheria za Makonda'.

Akizungumza na kipindi cha Dira ya dunia cha BBC, Mkuu huyo wa Mkoa huo amesema jambo hilo na anaamini kuwa ni hatua ambayo itakuwa mwarobaini wa changamoto za mahusiano katika jamii.

Kumekuwa na gumzo baada ya Makonda kutoa tangazo kuhusu mpango huo wa kuzisajili ndoa zote za mkoa huo kwa ajili ya kukabiliana na wanaume wanaowalaghai wanawake kimapenzi.

''Kama kiongozi unapata habari tofauti tofauti wananchi wakitoa mawazo yao,changamoto zilizopo na moja kati ya kazi tulizonazo ni kufikiri njia bora zaidi katika kutatua''.

Makonda amesema lengo lao ni moja tu, ni kutokuwepo kwa mtu kuingia kwenye makubaliano bila kuwa taarifa kuhusu mwenza wake.''Kwa mujibu wa Makonda, sheria ya Ndoa inampa mwanamke haki ya kwenda mahakamani na akalipwa fidia kutokana na hasara aliyoipata kwa ule muda aliopotezewa na mwanaume.

''Hii sheria ya ndoa imekuwepo siku zote sio sheria ya Makonda imetungwa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni suala la kuelimisha tu Umma kuhusu haki alizonazo mwanamke anapokuwa amerubuniwa na mwanaume''.Alisema.

''Watu ambao wanaingia kwenye hayo mahusiano wanajikuta wanapata watoto na mwisho wa siku Baba hata akifariki mtoto akipelekwa kwenye msiba hukataliwa na kufukuzwa kama mtoto asiyestahili hata kumuaga hata baba yake''.