Loading...

8/14/2019

Waendesha Bodaboda na Bajaji wafanya maandamano mbele ya RC Mwanri


Na Rahel Nyabali-Tabora

Umoja wa waendesha Bajaji na Bodaboda mkoani Tabora wamefanya maandamano ya amani kuhamasisha zoezi la uchangiaji damu kwa ajili ya waathirika wa ajali ya moto iliyotokea August 10  na kusababisha vifo vya watu wengi mkoani Morogoro.

Mwenyekiti wa waendesha Bajaji mkoa wa Tabora, Said Maganga amesema wameona ni vyema kuunganisha nguvu kuhamasisha jamii kuona umuhimu wa zoezi hili la uchangiaji damu kwani itasaidia kuokoa maisha ya majeruhi wa ajali .

“Tulipokea kwa mshituko tulipopata taarifa ya ajali hii, tumeona ni vyema kuungana na wenzetu kwa kutoa damu na tumepata fonzo kubwa kwa vijana  tuwe na moyo wa kujitolea ili kuweza kusaidia majeruhi wa ajali” amesema Maganga.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri pamoja na viongozi  wa dini akiwemo Isack lazier, Askofu kanisa la KKKT Dayosisi ya Magharibi wametoa wito kwa makundi  mbali mbali  kujitokeza kuendelea kushiriki zoezi hilo la uchangiaji damu ili kusaidia majeruhi  wa ajali hiyo.KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger