Wajumbe kutoka nchi zaidi ya 60 wanakutana mjini Lima, Peru, kujadili hatua za kuzuia mgogoro nchini Venezuela, wakati ambapo Marekani inaimarisha shinikizo la kumtaka Rais Nicolas Maduro wa nchi hiyo ajiuzulu.
Mkutano huo unafanyika siku moja baada ya Rais Donald Trump kuamuru kuzuia mali zote za serikali ya Venezuela zilizoko nchini Marekani na kuzuia miamala yoyote na viongozi wa serikali ya Venezuela.
Rais Trump amechukua hatua hiyo kutokana na Rais Maduro kuendeleza kile ambacho Marekani inakiita kupora mamlaka.
Mkutano huo umeitishwa na kundi la Lima la nchi kadhaa za Amerika ya Kati na Canada zinazojaribu kutafuta usuluhishi wa mgogoro wa Venezuela.
Mshauri wa usalama wa Marekani, John Bolton, pamoja na waziri wa biashara wa nchi hiyo, Wilbur Ross, ni miongoni mwa wajumbe wa Marekani wanaotarajiwa kutangaza hatua zaidi kwenye mkutano huo, hatua za kumwadhibu Maduro.
Venezuela ambayo ni nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta ilitumbukia katika mgogoro baada ya kiongozi wa bunge na upinzani, Juan Guado, kujitangaza rais wa kipindi cha mpito mnamo mwezi Januari.