Na Ahmad Mmow, Lindi.
Mkuu wa wilaya ya Liwale, Sarah Chiwamba ameutaka Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) kupambana kikamilifu kudhibiti uharibifu wa misitu katika wilaya hiyo.
Chiwamba ameeleza hayo mbele ya naibu wa wizara ya Maliasili na utalii, Constantine Kinyasu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maonesho ya wakulima( Nanenane) kanda ya Kusini.
Yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo, manispaa ya Lindi.
Chiwamba ambae alisema hayo wakati naibu waziri Kanyasu akipokea maelezo katika banda la Maliasili, alibainisha kwamba katika wilaya yake kuna uharibufu mkubwa wa misitu unaosababishwa na moto na ukataji miti holela.
DC Chiwamba bila kutafuna maneno alisema nijambo la kusikitisha kuona misitu mingi inayoharibiwa ni ile ya serikali kuu. Ambayo wasimamizi na watunzaji wake ni TFS.
'' Mheshimiwa waziri, ukienda Liwale unaweza kulia kutokana na uharibifu mkubwa wa misitu. Tunawezaje kuzalisha hiyo asali kwa wingi wakati misitu inateketea kwa moto!! ,'' alishangaa Chiwamba.
Kutokana na hali ya uharibifu wa misitu uliopo wilayani huo, alisema TFS hainabudi kufanya doria mara kwa mara. Akibainisha kwamba miongoni mwasababu zinazochangia uharibifu huo ni kukosekana doria za mara kwa mara.
Kwaupande wake naibu waziri Kinyasu alisema TFS imepewa dhamana ya kusimamia na kuendeleza misitu ya serikali. Hivyo inawajibu wa kuhakikisha hairibiwi.
Waziri huyo nae aliwanyooshea kidole cha lawama wakulima, hasa wa ufuta katika mkoa wa Lindi. Alisema wanamchango mkubwa katika uharibifu wa misitu kutokana na tabia ya kuanzisha mashamba mapya kila msimu wa kilimo.
Kinyasu aliwataka wakulima wa zao hilo wenyetabia hiyo na hata wengine wanaolima mazao ya aina nyingine waache tabia hiyo.
