Waziri Mkuu kuwa mgeni rasmi siku ya Kimataifa ya vijana


Na. Ezekiel Mtonyole, Dodoma 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka ishirini (20)ya siku ya kimataifa ya vijana kwa mwaka 2019 ambayo yatafanyika Jijini  Dodoma.

Akitoa taarifa kwa wanahabari,  Meneja Program ya Vijana na Maendeleo kutoka UNFPA- Tanzania Dkt Majaaliwa Marwa, amesema katika maadhimisho yanayowezeshwa na UNFPA, UNESCO, ILO na UNIC yanalengo la kuhakikisha vijana wanajengewa uwezo na kuwa na ubunifu mbalimbali.

Amesema maadhimisho hayo yatashirikisha vijana zaidi ya mia tano(500) kutoka Tanzania bara na visiwani na kwa mwaka huu wamejikita zaidi katika kutilia mkazo kuhusu elimu kwa vijana.

“Mwaka huu ni maadhimisho ya ishirini ya siku ya vijana kimataifa na mwaka huu tumejikita katika elimu ili kuwajengea vijana uwezo na kuwa wabunifu kuweza kujitegemea, dhamira Tanzania  iliyopendekezwa kuelekea 2030 Tanzania ya viwanda boresha elimu kwa ajiri ya maendeleo ya vijana” amesema.

Aidha amebainisha baadhi ya shughuri ambao zitafanyika jijini Dodoma ikiwa ni katika kudhimisha siku hiyo katika maeneo mbalimbali Jijini Dodoma.

“Tarehe 15 tutakuwa na kongamano litakuwa na maada mabalimbali ikihusisha ubunifu na afya ya uzazi kwa vijana, na siku ya pili kutakuwa na tamasha litakuwa katika eneo la Chang’ombe eneo  lenye mkusanyiko wa vijana wengi na kutakuwa na burudani nyingi” amesema.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Shirika la RESLESS DEVELOPMENT, chini ya mradi  wa Kijana wajibika  kwa mkoa wa Dodoma, Ridhiwani Juma, amesema wao kama wenyeji wameweza kuratibu na kuhakikisha hata vijana wenye mahitaji maalumu nao wanakuwa sehemu ya mmaadhimisho hayo.

Muwakilishi wa vijana ambaye ni katibu Afriyan Tanzania, Seif Ibrahimu amesema kundi la vijana linakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kiasi kikubwa.   
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items