Loading...

9/11/2019

Afya ya Askofu Mkuu wa Jimbo la Katoliki Dar yaimarika


Hali ya Askofu Mkuu wa Jimbo la Katoliki Dar es salaam, Mhashamu Yuda Ruwaichi inaendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa ubongo.

Daktari Bingwa wa Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Profesa Joseph Kahamba anasema Askofu Ruwaichi alikutwa na tatizo la damu kuvuja kwenye ubongo linaloitwa Chronic Subdural Haematoma.

"Aliletwa alikuwa tayari alifanyiwa upasuaji KCMC wao waliona anahitaji matibabu zaidi hivyo alivyo kuja alifanyiwa upasuaji na madaktari bingwa watatu."

“Hata hivyo timu ya wahudumu wa afya saba wako wanampatia matibabu lakini mpaka sasa hali yake inaendelea vizuri,anajitambua, anaongea na pia anaeleza hivyo kwa ujumla hali yake inaendelea vizuri,” amesema Profesa Kahamba.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger