Binadamu ana macho aina mbili. Macho ya nje kwa ajili ya kutazama vitu vya nje (sight) ambavyo watu wote wenye macho wanaona, na macho ya ndani kwa ajili ya kumsaidia kutazama mambo ya ndani (mtazamo) ambayo kila mmoja amepewa kuona vitu ambavyo haviwezi kuonekana kwa namna ya macho ya kawaida.
Mtu kuwa kipofu wa macho ya nje haimaanishi kuwa mtu huyo ni kipofu wa macho ya ndani pia. Ziko shuhuda kubwa duniani za watu wenye ulemavu wa macho ambao wamefanya mambo makubwa kuliko hata watu wenye macho. Upungufu mkubwa tunaopaswa kuogopa siyo ulemavu wa macho ya nje bali ulemavu wa macho ya ndani au mtazamo ambacho ndicho kitu hatari sana kwa mstakabali wa maisha ya binadamu anachopaswa kuogopa sana.
Nchini India kuna kijana mwenye ulemavu wa macho ambaye anatingisha dunia kwa sasa. Historia yake yote ni hadithi inayovutia na kusisimua kila anaesikiliza. Katika umri wa miaka 27, Srikanth Bolla tayari anamiliki kampuni yenye utajiri wa zaidi ya dola 16 milioni.
Alizaliwa katika familia maskini akiwa kipofu. Maisha yake ya utoto aliishi kwa kutengwa na unyanyapaa mkubwa. Wana kijiji waliwashauri wazazi wake wamuache afe kwa kuwa alikuwa kipofu. Wazazi wake hawakutaka kusikiliza ushauri huo wa hovyo lakini ubaguzi uliendelea kumwandama hata alipokuwa shule safari yake ilikuwa ni ya upweke mkubwa.
Jamii ilimhukumu kwa kutumia ushahidi wa nje ambao hauna nguvu eti kwa kuwa alikuwa kipofu kana kwamba upofu ule uligusa utu wake wa ndani na kwa maana hiyo hawakuona kuwa kuna kitu chochote ambacho angeweza kufanya maishani mwake.
Dunia iliamini kuwa yeye ni kipofu masomo ambayo angeweza kufanya ni yale ya sanaa tu lakini yeye alikataa kwa kuwa kiu yake ilikuwa ni kusoma masomo ya uhandisi na alinuia kujiunga na chuo kikuu maarufu nchini India cha Teknolojia ya mawasiliano nako walimkatalia kutokana na hali yake.
Kijana huyu hakukubaliana kabisa na hukumu ya uongo iliyokuwa inatolewa na jamii juu yake. Alikataa kwa sababu mtu wa ndani mwake alikuwa hajulikani na kazi ya kumtambulisha alijua inamhusu yeye mwenyewe. Alipambana na unyanyapaa mpaka aliposhinda na kufanikiwa kufika alikokuwa anakusudia.
Ni vipofu wangapi umekutana nao na kushindwa kuwapa heshima wanayostahili kwa kigezo cha kupoteza uono wao wa macho tu? Ni vipofu wangapi umeshiriki kuua ndoto zao kwa kuwahukumu vibaya? Ni vipofu au walemavu wangapi wamekufa bila kuongeza thamani katika kijiji alichozaliwa Srikanth Bolla kabla hajajitoa muhanga kubadilisha hali hiyo katika jamii?
Utashangaa utakapogundua kuwa idadi ya vipofu wasioona kwa macho ya ndani ni wengi kuliko vipofu wasiokuwa na macho ya kuona kwa macho ya nje. Wapo watu wengi vipofu wa macho wenye akili na hekima kubwa kuliko watu wengi wenye macho ingawa dunia haiwapi nafasi.
Kuna wakati unapaswa kusimama kidete kujitetea na kujitambulisha mwenyewe, hata kama dunia nzima haikuelewi ni kazi yako kujitambulisha mpaka itakapofikia unaeleweka na kuanza kutumia uwezo ule mkubwa uliofichika ndani mwako.
Mwandishi wa Napoleon Hill aliyendika kitabu maarufu cha “Think and Grow Rich” anasisitiza hili kwa nukuu yake “It takes half of your life before you discover life is a do-it- yourself project” Anasema inamchukua mtu nusu ya maisha yake kabla ya kugundua kwamba maisha ni mradi wa kufanya mwenyewe. Kama ndivyo iweje ukubaliane na maoni ya watu ambao hawana hata uzoefu wa nusu ya maisha yako tangu wakufahamu?
Srikanth alifungua kesi katika tume ya vyuo vikuu na baada ya kusubiri miezi sita majibu yalirudi kuwa alishinda akaruhusiwa kujiunga na chuo kikuu. Kutokana na ubaguzi aliamua kutafuta chuo nje ya nchi na akafanikiwa kusoma masomo yake ya shahada katika chuo kikuu kimoja cha uhandisi huko Boston Marekani akiwa mlemavu wa kwanza wa aina yake kuhitimu shahada chuoni hapo.
Baada ya kuhitimu shahada yake alipewa nafasi ya kufanya kazi huko Marekani lakini yeye alisema hahitaji kuajiriwa kwa kuwa ndani mwake hakuna kabisa kinasaba cha kuajiriwa aliamua kuwa anarudi India na pengine angefikiria kurudi nchini Marekani siku za usoni kama angeamua kuchukua shahada ya juu kama atakuwa hajawa raisi wa kwanza mlemavu wa India kama anavyoamini.
Utaona kabla ya kuwa maarufu alikutana na changamoto nyingi kama wanazokutana nazo walemavu wengi.Bila kutambua kusudi alilokuwa amebeba ndani mwake angeshindwa mapema. Kudharauliwa na kupuuzwa sana katika jamii nchini mwake na kuhukumiwa kuwa ni mtu ambaye hangeweza kufanya kitu kutokana tu na jinsi alivyoumbwa. Mfumo wa elimu wa India haukuwa tayari kumsaidia asome ili aweze kutimiza ndoto na kusudi la kuwepo kwake duniani.
Alichokuwa amebeba ndani mwake ni wito mkubwa wa kuwepo kwake hapa duniani kusaidia jamii ya watu wanaodharaulika katika jamii ikiwemo walemavu. Leo hii ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni kubwa inayoajiri maelfu ya walemavu na watu wasio na elimu huko India.Baada ya miaka mingi dunia inapata nafasi ya kuona kile alichokuwa anaona ndani mwake tangu utoto ambacho macho ya watu wengine yalikuwa hayaoni.Bila kun’gan’gana nani angemjua leo?
Changamoto au kushindwa unakopitia ni kama mtihani wa maisha na lengo la mwalimu kumtungia mwanafunzi mtihani huwa ni kupima uelewa wake kujua kama alichofundisha kimeeleweka. Hakuna mkufunzi mwenye akili timamu anayefurahi eti kwa sababu mwanafunzi wake ameshindwa mtihani aliomtungia.
Hakuna changamoto maishani inayokuja kwa lengo la kumtoa mtu kwenye mstari wa maisha la hasha. Changamoto ni kama fursa kwa ajili ya kumpima mtu na kumvusha kutoka hatua ya moja kwenda nyingine. Watu wanaotafuta kushindwa wanaita changamoto matatizi na wale wanaotafuta ushindi wanaita changamoto.
Naamini utakuwa umepata kitu kupitia makala hii fupi.

Tags:
makala