Kamati ya Bunge yazitaka Halmashauri kutegua kitendawili kigumu


Na Ahmad Mmow, Lindi

Halmashauri nchini zimetakiwa kutafuta sababu na kupata suluhisho la kudumu la tatizo la wanaume wengi wanaoishi na virusi  vya UKIMWI (VVU) kushindwa kujiunga kwenye vikundi maalumu  vya uzalishaji mali vya watu wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI.

Wito huo ulitolewa jana na mwenyekiti wa ya kamati ya kudumu ya bunge la Jamuhuri ya Tanzania inayoshughulikia UKIMWI, kifua kikuu( TB) na dawa za kulevya, Osca  Mukasa katika kijiji cha Namichiga, wilaya ya Ruangwa. Baada ya kutembelea kikundi cha uzalishaji mali cha watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI.

Alisema vikundi vingi vya aina hiyo vinawanaume wachache kuliko wanawake. Hali inayohitaji utafiti ili kujua sababu na njia za kuondoa hali hiyo ambayo alifanisha na moto mkali unataka kulipuka na kusàbabisha madhara makubwà kwa jamii.

Alisema ili kuzuia màdhàra hàyo yasitokee  nimuhimu halmàshàuri zitafute sababu za wanaume wengi kushindwa kujiunga na vikundi hivyo ambavyo uwepo wake unarahisisha kufikishiwa misaada na mikopo kutoka kwa Sarah mbalimbali. Ikiwamo tume ya kudhibiti UKIMWI( TACADIS).

"Umoja ndio nguzo ya mafanikio, TACAIDS na NACOFA( Baraza la taifa la watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI) kupitia hamashauri kaeni mtafute sababu na njia za kutatua changamoto hiyo," alisema Mukasa.

Mwenyekiti huyo alitoa wito kwa wanaume wanaoishi na virusi vya UKIMWI wajiunge katika vikundi hivyo ili wasiachwe nje. Kwani waathirika wa maambukizi mapya ni viiana, ambapo vijana wanaongoza ni wanawake. Kwahiyo hali hiyo isipodhibitiwa nisawa na moto au bomu unaotarajiwa kulipuka.

Aidha Mukasa ametoa wito kwa halmashauri nchini kutafuta na kubaini fursa mpya zinazoweza kutumiwa na vikundi hivyo.Badala ya kuwa miradi ya ufugaji pekee.Kwani miradi mingine ikiungana na ufugaji inaweza kupanua wigo wa uchumi wao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza wanaoishi na VVU, Leticia Moris aliiomba serikali kuendelea kutoa fedha  ili kuwezesha vikundi vingine zaidi  kuepuka utegemezi.