Kocha wa Malindi aahidi kuwashangaza mashabiki wake dhidi ya Al Masr



Na Thabit Madai,Zanzibar.

KOCHA wa Timu ya Malindi SC, Saleh Ahmed Machupa amewaahidi mashibiki wa timu hiyo  kufanya vizuri katika mchezo wa kwanza raundi ya Pili  kombe la Shirikisho barani Afrika Dhidi ya timu ya Al Masr kutoka Nchini Misri.

Kocha Machupa alitoa kauli Kauli leo wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuelekea mchezo wao huo siku ya  kesho katika Dimba la Amani Stadium majira ya saa 10:00 jioni.

Kocha Machupa alisema licha ya wapindani wao Al Masr kuwa na uzoefu wa muda mrefu katika mashindano ya kimataifa lakini anawaahidi mashabiki wa timu hiyo kufanya vizuri na uibuka na ushindi na kutinga hatua inayofuata.

“Kiukweli kuwa Al Masr ni timu kubwa barani afrika lakini  nina imani na timu yangu kufanya vizuri  kutokana na maandalizi tulioyafanya na aina ya wachezaji ambao tunao kwa wakati huu” alisema Kocha Machupa.

Alisema licha kuwa wanamajeruhi watatu anaamini kuwa watafanya vyema sababu anakikosi kipana ambacho kitaziba mapengo ya wachezaji hao.

Aidha kocha Machupa alisema kuwa anaimani kuwa Timu ya Al Masr wanahofu na Malini hivyo watumia udhaifu kuweza kupata matokeo yalikuwa mazuri.

Nae Nahodha wa Timu ya Malindi SC Ali Kan Mkanga aliaomba mshabiki na wapenzi wa soka viswani Zanzibar kujitokeza kwa ingi kuwapanga nguvu wawakilishi hao wa Zanzibar katika mashindao ya kimataifa.

“Tuna amini mchezo utakuwa mgumu kwa timu zote, kikubwa niwaombe mshabiki wa Soka wajitokeza kwa wingi kuja kuutunga mkono ukizingati Malindi SC ndo Timu pekee iliyobaki kuiwakilisha Zanzibar kimataifa”alisema Nahodha wa Timu hiyo.

Kwa Upande wa Kocha Mkuu wa Timu ya Al Masr IHAB Galal alisema kuwa hadi sasa timu yake ipo vizuri kuelekea katika mchezo huo hapo kesho na wamejipanga kupata matokeo mazuri na kuendelea na hatua inayofuta.

“Malindi SC si timu ya kudharau tumewaona uwezo woa wa michezo miwili ambayo wamecheza ila sisi tumeshauona udhaifu wao na tunajipnga kupat matokeo mazuri” aisema Kocha Mkuu wa Al Masr.

Katika maelezo yake alielea kuwa timu yake ina mchezaji mmoja tu amabaye hayupo sawa kiafya na ambapo atakosa mchezo wa kesho.