Na James Timber Mwanza
Mkazi wa Kitongoji Cha Bulolo B Kijiji Cha Bulolo Kata ya Iligamba Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza Daniel Madafu (45) ambaye ni Mwenyekiti wa kitongoji hicho amenusurika kifo baada ya kufanyiwa upasuaji mara mbili ndani ya miaka miwili.
Akipiga story na Muungwana Blog, Madafu kuwa mwaka 2018 aliugua gafla akiwa matembezini na kukimbizwa kituo Cha afya Cha Mwanangika na alipofika baada ya kupigwa aliambiwa kuwa anatatizo la bandama kuwa imeharibika ndipo madaktari walipo mfanyia upasuaji na kuondoa bandama hiyo.
Baada ya kutolewa bandama hiyo alirejea nyumbani wakati akiwa Bado anauguza kidonda Hali ilibadilika Tena mwaka huu 2019 mwezi wa 8 ambapo alivimba tena tumbo na kitovu na kupelekwa kituo Cha afya Cha Mwangika Kisha kufanyiwa upasuaji na kukutwa utumbo mpana umejikunja na wakati akifanyiwa hivyo tumboni mwake walitoa takribani ndoo mbili za maji ambapo kila mmoja alistaajabu.
Kulingana na Hali hiyo anawaomba wasamalia wema kujitokeza kumusaidia ili aweze kuendesha familia yake kwa kuwa kwa Sasa Hanna uwezo wowote kutokana n Hali aliyonayo.
'"Ninawaomba watanzania wenzangu munisaidie ninafamilia ya watoto Saba Mali zote nimeuza kutokana na maradhi yaliyonipata Sina namna yoyote Bali naomba msaada ''alisema , Madafu.
Mtoto mkubwa na baba huyo aitwaye Edward Madafu ambaye anasoma chuo Cha ufundi jijini Mwanza amesema kuwa ugonjwa
wa baba yake unameathiri kimasomo kutokana na yeye kukatisha masomo yake na kulejea nyumbani ili amhudumie baba yake.
Anaiomba serikali ,asasi za kiraia na watanzania kwa ujmla kujitokeza kuwasaidia kutokana na ukata walionao familia hiyo ambayo ni masikini.
''Hatukutegemea kama baba atakuwa kama alivyo leo kumbe tunapaswa kujua afya ya binadamu hubadilika kila kukicha tunaomba mtusaidiwe '' alisema. Edward.
Thomas Malima ambaye ni jirani wa familia hiyo alisema kuwa familia hiyo imekumbwa na matatizo mbalimbali kutokana na baba wa familia hiyo na mama wa familia hiyo kuugua na watoto kuhangaika.
Malima amesema kuwa amekuwa akitoa msaada wa kuwapeleka kwenye huduma ya matibabu I kila Mara na kutoa huduma ya chakula hivyo peke yake hawezi hivyo anawaomba wasamalia wema kumsaidia.
Mama wafamilia hiyo tatu maganiko ambaye naye ni mgonjwa wa miguu baada ya kujifugua amesema familia yao iko katika mazingira magumu na kuiomba serika ijitokeze kuwa saidia.
Diwani wa kata ya Iligamba Mlamba Maboni amesema kuwa atahamasisha wananchi waweze kumsaidia ili aweze kuendesha maisha yake na kuendelea kupata matibabu zaidi.
