Loading...

9/13/2019

Raia wa Nigeria warejea nchini kwao kutokea Afrika ya kusini

Kufutia mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni wenye asili ya Afrika na haswa raia wa Nigeria nchini Afrika kusini, raia wa Nigeria wapatao 200 wamerejea nchini kwao.

Mwenyekiti wa baraza la Diaspora la Nijeria (NIDCOM) Abike Dabiri-Erewa ametoa taarifa kuwaambia wana habari kwamba raia wa Nijeria wapatao 189 waliokuwa wakisubiri kurejea makwao kwa zaidi ya masaa 15 katika uwanja wa ndege wa Johannesburg hatimaye wamerejea nchini kwao.

Dabiri-Erewa amesema kufuatia ukatili na mashambulizi dhidi yao nchini Afrika kusini raia wa Nijeria 640 wameomba  kurejea nchini kwao,raia wengine waliobaki nchini humo waliomba kurejeshwa kwao watasafirishwa siku nyingine.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger