Rais wa kwanza wa Zimbabwe ambaye ni muasisi na Baba wa Taifa hilo, Robert Mugabe amefariki dunia hii leo akiwa na umri wa miaka 95.
Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amethibitisha kifo cha Mugabe kupitia akaunti yake ya Twitter.
“Kwa majonzi makubwa, natangaza kifo cha Muasisi na Baba wa Taifa la Zimbabwe, Robert Mugabe,” amesema Rais Mnangagwa.
Ikumbukwe hapo awali Rais huyo wa Zimbabwe aliliambia Taifa hilo kuwa Mugabe alikuwa anasumbuliwa na maradhi pamoja na uzee ambapo.
Alikuwa Rais wa Zimbabwe tangu mwaka 1980 hadi mwaka 2017 alipolazimika kujiuzulu. Mugabe alizaliwa Februari 21, 1924 kwenye koloni la Rhodesia.
Alitupwa jela kwa miaka 10 bila ya kufunguliwa mashtaka kwa kuukosoa uongozi wa Rhodesia mwaka 1964. Mwaka 1973, yungali gerezani alichaguliwa kuwa raisi wa chama cha Zimbabwe African Union (Zanu), ambacho alikuwa ni mwanachama mwanzilishi.
