Sababau za kujua kitu unachokipenda

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kufanya kitu kwasababu unakipenda, au kwasababu unapendelea kukifanya kwasababu kinakupa fedha. Nimekua nikijiuliza maswali mengi siku hizi za karibuni, hivi kitu gani nikikifanya kina nipa furaha na uhuru ule wa  ndani yangu, na kila ninapojiuliza ndipo nakaribia kujua kitu gani hasa napendelea.

Ukijaribu kuangalia, ndani yako utagundua kuwa kuna vitu huvipendi, na kuna vitu unavipenda, na hii ipo katika maeneo yote ya maisha. Ili uweze kuishi kwa amani, ni lazima ujue kitu gani ukikifanya kinakupa furaha, mtu gani ukikaa nae chini ukazungumza nae, anakufanya upunguze labda uchovu, kukata tamaa n.k.

Kila mtu ana upekee wake na namna ambavyo anaweza kugusa maisha ya wengine au kuwafanya watambue ndoto zao, malengo yao, watu ambao wanataka kuwa nao kwa maisha yao yote n.k, unatakiwa ujue hiko kitu au huyo mtu ili uweze kuwa na ndoto za kutimiza, na sababu ya kuamka asubuhi kwenda kufanya kazi.

Ukisha jua huyo mtu ambae anaweza kukufanya utambue nini hasa kinakupa ule uhuru wa ndani yako na ile furaha ya kudumu, jaribu kutafuta kazi yako katika maisha haya, tatizo linalowafanya waafrika na watanzania wengi kutokufika mbali kimaendeleo ni kutokujua kitu gani hasa ni kazi zao hasa ambazo wanapaswa kuzifanya. Hii inatokana na mifumo ya elimu tuliyonayo lakini pia mawazo ambayo tumejiwekea, ya kusoma ili tuajiriwe badala yakusoma ili tupate ile furaha ya kufanya kitu tunachopendelea kukifanya. Sababu ya watu wengi wa njee kuendelea ni kuishi kwenye yale mambo ambayo kwanza wanayaweza lakini pili yanayowapa furaha.

Mfano ni Alicia Keys, Yeye alizaliwa tarehe 26 January mwaka 1981, na kuanza kujifunza muziki kwa kuchukua somo la kwaya kama soko kuu. Tangu ahitimu alipokua na umri wa miaka 7 mpaka sasa amekua akifanya muziki. Ni mwanamuziki aliyedumu kwa miaka mingi kwenye muziki bila ya kuwa na skendo za aina yeyote ile. Ni mwanamuziki mwenye mafanikio sana katika muziki lakini pia kujizolea tuzo nyingi kama za Bilbord, MTV music award, America music award n.k

Kitu chochote kile au ujuzi wowote ule ambao mtu anaamua kuuchukua, lengo kuu ni kupata uhakika wa kuishi maisha vizuri na kupata nafasi ya kuihudumia familia yake vyema. Hata sababu ya vijana wengi kukimbilia kwenye siasa kwa wingi kuliko sehemu nyengine ni kwasababu kwenye siasa kuna uhakika mkubwa au ulinzi mzuri wa kupata maisha bora kwa mtu binafsi na familia yake.

Lakini kitu ambacho wengi tunakisahau ni  kitu chochote ambacho utakifanya goal yako, kwa maana ya ndoto unayoifanyia kazi na kuiwekea ukomo kwamba, kutoka muda flani hadi muda flani nataka niwe nimefanikisha kitu flani, basi unaweza kupata ulinzi, uhakika au security ambayo unaitafuta kwenye mambo mengine yakiwemo kama siasa.