TFS yatoa mafunzo ya utunzaji wa rasilimali za Misitu


Wakala wa Huduma za Misitu Tazanania (TFS) imekutanisha watu wenye ulemavu wa kusikia maarufu viziwi kutoka mikoa mitano ya nyanda za juu kusini na kuwapa mafunzo ya kuwajengea uwezo katika utunzaji wa rasirimali za misiti na ufugaji nyuki ili kuwa na uwezo wa kuhimarisha kipato cha familia zao.

Hatua hiyo imekuja baada ya kundi hilo maalumu katika jamii za kitanzania kupaza sauti katika majukwaa ya umma wakidai taasisi nyingi za umma na binafsi zimekuwa zikiwatenga katika masuala mbalimbali ikiwemo kujumuishwa katika mafunzo yakuwaongezea ujuzi.

Akitoa ripoti ya utafiti ya 2015 iliyofanywa na TFS Kaimu Meneja wa Nyanda za juu Kusini, Ebrantino Mgiye amesema takribani hekta laki 275 za misitu zimeteketezwa nchini nyanda za juu kusini pekee ikionekana kuchangia asilimia 16 kutokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo kuchoma mkaa, kilimo na uchomaji wa mioto na kwamba kuliemisha kundi hilo muhimu kutasaidia kutunza mazingira yetu.

Mbali na kutoa elimu ya utunzaji wa rasilimali za misitu TFS imeanza kutoka mafunzo ya ufugaji nyuki kwa kundi hilo la walemavu ili waweze kuwa na uelewa kuhusu ufugaji huo ambapo utawapa fursa ya kutengeneza kipato.

Awali akifungua mafunzo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe , Dr George Katemba ambaye ni mkuu wa idara ya uchumi na uzalishaji amesema wakala huo wa misitu umefanya jambo la maana kulitambua kundi hilo maalumu na kulipa elimu ya utunzani wa rasirimali misitu na ufugaji nyuki kwa kuwa limekuwa na mchango mkubwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kelvin Nyema ambaye ni katibu mtendaji wa taasisi ya maendeleo kwa viziwi Tanzania TAMAVITA na Twasigwe Mwalegwa mlemavu wanasema nyanda za juu kusini imekuwa na uharibifu mkubwa wa mazingira na kwamba mafunzo hayo yatasaidia kutunza mazingira pamoja na kujiajiri katika kilimo cha nyuki .

Katika hatua nyingine watu hao wenye ulemavu wa kusikia wameziomba taasisi nyingine kulitambua kundo lao na kulipa kipaumbele kama makundi mengine pindi wanapotoa fursa zikiwemo za mafunzo na misaada mbalimbali.