https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mwalimu aliyetuhumiwa kumbaka mwanafunzi aachiwa huru | Muungwana BLOG

Mwalimu aliyetuhumiwa kumbaka mwanafunzi aachiwa huru


Mahakama ya Hakimu Kazi Mkoa wa Kigoma, imemwachilia huru kwa mara nyingine Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyantore, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Jason Rwekaza, aliyeachiliwa huru kwa mara ya kwanza Septembe 16 na kukamatwa tena Septemba 19 kwa tuhuma tatu za kumbaka na kumtia mimba mwanafunzi wake.

Rwekaza ameachiwa huru baada ya upande wa serikali kusema haina nia ya kuendelea na shitaka hilo.

Hakimu Elia Baha anasema amemwacha huru chini ya kifungu cha 91 kifungu kidogo cha kwanza cha mwenendo wa makosa ya jinai.