https://monetag.com/?ref_id=TTIb Wanamgambo wa Taliban walipua kituo cha umeme | Muungwana BLOG

Wanamgambo wa Taliban walipua kituo cha umeme


Wanamgambo wa Afghanistan wamelipua kituo cha umeme katika mkoa wa Salang mkoa wa mashariki mwa Parwan na kuuacha mji wa Kabul gizani.

Msemaji wa Polisi wa mkoa huo, Mohammad Salim Nuri akiongea na vyombo vya Habari amethibitisha kutokea kwa shambulio hilo.

"Wanamgambo wa Taliban walilipua kituo cha umeme katika mkoa wa Salang kilomita 70 kaskazini mwa mji wa Kabul hivi leo (Jumatano) mapema na hivyo kuacha mji wa Kabul gizani,"  alisema Nuri.