Watu watano wachomwa kisu katika maduka ya Manchester

Polisi ya kupambana na ugaidi wanachunguza tukio ambalo mtu aliwavamia watu na kuwachoma kisu kaskazini magharibi mwa Uingereza.

Watu watano walijeruhiwa katika tukio hilo na kupelekwa hospitali. Shambulizi hilo limetokea leo katika eneo la kibiashara la Arndale katikati mwa mji wa Manchester, ambako mlipuaji wa kujitoa mhanga aliwauwa watu 22 baada ya tamasha la muziki lilioandaliwa na mwanamuziki Ariana Grande mwaka wa 2017.

Mtu mmoja amekamatwa kuhusiana na tukio hilo. Video iliyosambaa kwenye intaneti ilionekana kumuonyesha afisa wa polisi akimdhibiti mshukiwa mmoja sakafuni huku mwingine akiwa amesimama kando yake.
Mpya zaidi Nzee zaidi