China yamhukumu kifungo cha maisha raia wa Japan

Mahakama moja kusini mwa China hii leo imemhukumu aliyekuwa mwanasiasa wa Japan kifungo cha maisha gerezani kwa ulanguzi wa dawa za kulevya zilizokuwa zimefichwa ndani ya sanduku alilokuwa akijaribu kulisafirisha hadi nchini mwake.

Mwanamume mmoja kutoka Mali pia alihukumiwa kifo huku mwengine kutoka Guinea akihukumiwa kifungo cha maisha kwa kupanga na kuwasilisha sanduku hilo. Hii ni kulingana na mahakama moja ya Guangzhou iliyoshughulikia kesi hiyo.

Takuma Sakuragi alikanusha mashtaka hayo na anapanga kukata rufaa. Hii ni kulingana na wakili wake mwenye makao yake mjini Guangzhou, Chen Weixiong ambaye anasema hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa Sakuragi alikuwa amebeba sanduku hilo huku akihamu kama amebeba dawa za kulevya.

Kulingana na Chen, rafiki yake kutoka Nigeria alimuomba Sakuragi kumpelekea sanduku hilo nchini Japan lililoonekana kujaa viatu.
Mpya zaidi Nzee zaidi