Watafiti nchini watakiwa kuhakikisha tafiti wanazofanya zinasaidia katika kutengeneza sera


Watafiti nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa tafiti wanazofanya zinasaidia katika kutengeneza sera au kuziboresha ili kutoa mchango wa moja kwa moja kwa jamii na taifa badala ya kuishia kwenye makabati na machapisho ya kimataifa.

Wito huo umetolewa na Naibu waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile wakati akifungua Mkutano wa mwaka nakongamano la Kisayansi la chama chaMadaktari wa mifugo Tanzania (TVA)uliokutanisha wadau wote wa Afya moja kutoka wizara,Taasisi za elimu yajuu, Taasisi za utafiti, Mashirika ya Kiserikali na yasiyo ya Kiserikali kutoka Tanzania na nje ya Tanzania uliofanyika kwene ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items