Wizara ya afya na Shirika la Msalaba Mwekundu watoa Elimu kuhusu Ebola


Na George Bahemu Ngara-Kagera

Wananchi wa wilayani Ngara mkoani Kagera wamepewa Elimu namna gani yakujikinga na mlipuko wa ugongwa wa Ebola ambao umeonekana kuwa tishio nchi za jirani kama DR Congo.

Wakizungumza na Muungwana Blog baadhi ya wananchi hao wamesema wamefurahishwa na semina hio kwani wamejifunza namna gani ya kujikinga na ugongwa huo ambao umekuwa tishio nchi jirani.

Mwenyekiti wa ulinzi na usalama wilayani Ngara mkoa wa Kagera, Luteni kanali Machael Mtenjele ambaye amewataka wananchi kuchukua tahadhari mapema nakuwapima wageni wanaotokea nchi jirani kama Burundi ambayo inapatikana wilayani humo ambapo Burundi ni jirani na Kabanga na Benaco ambapo ni jirani na Rwanda.

Dr Meshack Nyeri ambaye anatokea wizara ya afya idara ya Kinga kitengo cha Elimu ya afya kwa umama amesema kuwa lengo la kutoa elimu hiyo ni jinsi gani wananchi wanaweza kujikinga na Ebola nakutembelea jamii ambazo ziko mpakani kwani ni pamoja na DR Congo ambayo ni nchi inayokumbwa na ungonjwa huo kwakiasi kikubwa.

"Bora leo tumekutana na wahudumu wa afya ngazi ya jamii ambao watakuwa kama wajumbe watakaofikisha ujumbe kwenye jamii na baada ya hapo tutaenda mpakani kuongea na wananchi wa huko kuwapa elimu pia jinsi gani watajikinga na Ebola." amesema Dr Meshack

Loti Bihagila ambaye ni Mkurugenzi wa Red Cross lakini pia ambaye ni mratibu wa shughuli za red cross mkoa wa Kagera amesema lengo lao kutoa elimu ni kufundisha namna gani mwananchi anaweza kujikinga na ugonjwa huo ambao umeonekana kuwatishio kubwa.

Hata hivyo amesema baada ya elimu hiyo kuna nyezo ambazo watazitoa kwaajili ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii ili kwenda kutoa elimu na kuna mashine ambayo inatarajia kupatikana ili kupima joto la ugongwa huo na mtu ambaye atakuwa na joto kubwa itaashiria kuwa ameambukizwa ugonjwa huo.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items