Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey
Polepole amemwambia Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye uwa alimueleza
asingeweza kupata kazi ya kushauri chama chochote cha siasa kama
angekuwa nje ya Chama Cha Mapinduzi.
Polepole ametoa kauli hiyi saa chache baada ya Waziri Mkuu Mstaafu
Frederick Sumaye kutangaza nia yake kujiondoa ndani ya CHADEMA kwa kile
alichokidai kuwa hakuna demokrasia ya kweli.
Polepole ameandika kupitia akaunti yake ya Twitter na Instagram "
Mzee
nilikwambia, kazi ya ushauri hutaipata ukiwa nje ya CCM wenzako
wanaotushauri na tunazingatia ushauri wao kwasababu tunawaheshimu, ni
wana CCM na kiitikadi tuko pamoja. Sasa umebaki bila Itikadi. Ile ni
mali ya Mtu ni yake, nilikwambia mwache, ona sasa unahama mara ya pili,”
ameandika Polepole.
Akitangaza
uamuzi wa kujiondoa CHADEMA Waziri Mkuu Mstaafu Sumaye amesema kuwa
“baada ya kutafakari kwa kina, ustaarabu unasema toka sasa hutakiwi,
wako watakaosikitika nimelazimika kujiondoa CHADEMA kutoka leo hii, mimi
sio Mwanachama wa CHADEMA na sijiungi na chama chochote, ila niko
tayari kutumika na chama chochote”