Loading...

12/04/2019

Sumaye akanusha kupewa fedha ili kuondoka CHADEMA


Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania, Frederick Sumaye amesema hajapewa fedha ili kuondoka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kusalia bila chama cha siasa kwa sasa.

Akizungumza na Wanahabari leo Dar es Salaam amesema kuwa alijiunga na chama hicho bila kupewa fedha na ndivyo ameondoka. 

"Najua katika kujikosha yatakuwepo maneno Kama kapewa fedha na CCM au ACT n.k, kama nilipokuja CHADEMA nilipewa pesa basi na safari hii nimepewa fedha ingawa sijui na nani maana sijiungi na Chama chochote” amesema.

“Na kama nilikuja CHADEMA kwa hiari yangu bila kupewa pesa basi na safari hii sijapewa pesa na sitopewa pesa maana sijiungi na Chama chochote, mimi sijawahi kuwa Kibaraka wa Mtu wala Kikundi na hata siku moja sitokuwa hivyo” amesitiza.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger