Loading...

1/16/2020

Hali ya jangwani bado mbaya barabara yafungwa

Hali halisi eneo la jangwani, mamlaka zimefunga rasmi matumizi ya barabara ya Morogoro eneo la magomeni kuelekea katikati ya jiji kufuatia kujaa kwa maji eneo la jangwani.

Kwa hali hiyo imesababisha msongamano mkubwa karibu maeneo yote ya jiji ambapo njia ya kuelekea Kinondoni Mkwajuni eneo la Magomeni Morocco  pia maji yamejaa na msongamano wa magari na watu ni mkubwa pia.

Katika hali nyingine Basi la kampuni ya Tahmeed limekwama  katika eneo la jangwani baada ya kujaribu kukatisha wakati wa maji hayo yakiwa tayari yamejaa.

Baadhi ya wananchi wametoa wito kwa kuiomba Serikali kuhakikisha wanaleta mpango maalum wa  daraja utakaosaidia kuondoa usumbufu wanaopata kila wakati wa eneo hilo linapojaa maji.

Barabara hiyi imefungwa kuanzia majira ya saa 12 asubuhi ambapo jeshi la Polisi limeweka ulinzi mkali kwa raia kutokatisha eneo hilo.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger