IGP Siro kesho kuwatunuku shahada na stashahada askari polisi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro  kesho  Januari 24, 2020 atatunuku askari Polisi Stashahada 140 na Astashahada 183  za taaluma na ujuzi wa Sayansi ya Polisi katika Mahafali ya nne ya Vyuo vya Polisi Tanzania.

Mahafali hayo  ni ya nne kufanyika katika vyuo  vya Polisi Tanzania ambayo yatahusisha vyuo  vinne vya polisi ambavyo ni  Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA), Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu (TPSC), Chuo cha Polisi Zanzibar ( ZPC) na Shule ya Polisi Tanzania ( TPS).

Katika mahafali  hayo  IGP Sirro  atawatunuku  stashahada   ya upelelezi wa makosa ya jinai 101 kutoka Chuo  cha maafisa wa Polisi Kidatu,  stashahada ya sayansi ya polisi  39 kutoka Chuo cha taaluma ya Polisi Dar es salaam,

Astashahada nyingine ni astashahada ya ujuzi wa upelelezi wa makosa ya jinai 88 kutoka Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu, astashahada ya  ujuzi  wa Sayansi ya Polisi 18 kutoka shule ya Polisi Tanzania, Astashahada ya  Mawasiliano ya Polisi  18 kutoka shule ya polisi Tanzania, na cheti cha awali cha Sayansi ya Polisi 59  kutoka shule ya Polisi Tanzania.

Mahafali hayo yatapambwa na burudani mbalimbali  ikiwemo gwaride maalumu  pamoja na maandamano ya wanataaluma na  bodi ya ushauri ya mafunzo ya Jeshi la Polisi.

Mpya zaidi Nzee zaidi