Na Amiri kilagalila-Njombe
Baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe limepokea na kupitisha bajeti ya zaidi Bilioni 35.56 ambazo halmashauri imepanga kukusanya na kutumia katika mpango na bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
Awali akiwasilisha rasimu ya mpango wa bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2020-2021,kaimu mchumi wa halmashauri Emma Lunojo amesema,kati ya fedha hizo kati yake mapato halisi ya ndani ni shilingi bilioni 4.1 kutoka bilioni 3 kwa mwaka wa fedha 2019/2020, ongezeko litokanalo na ukamilishaji wa miundombinu ya ujenzi wa stendi kuu ya mabasi,upanuzi wa masoko ya mbao na ujenzi wa soko kuu.
“Mapendekezo yaliyotolewa baraza liidhinishe jumla ya shilingi bilioni 35 milioni 560 laki saba sabini na mbili na 226 tu,kati yake mapato halisi ya ndani ni shilingi bilioni 4 milioni 191 laki nane na kumi na nne,ruzuku ya mishahara shilingi bilioni 25 milioni 571 na laki tisa 80 huku ruzuku ya miradi ya maendeleo ni shilingi bilioni 3 milioni 106 laki 7 na hamsini na nane na 722,ruzuku ya matumizi mengineyo ni shilingi milioni 895 laki tano na 24 tu na michango ya wananchi ikiwa bilioni 2 milioni 690,laki mbili 19 na mia tano na nne”amesema Emma Lunojo
Amesema ongezeko la wigo wa mapato ya ndani litaipa halmashauri uwezo wa kuendelea kuwekeza kwenye miradi mingine yenye kuongeza vyanzo vya mapato kwa Halmashauri na huduma kwa Wananchi ambapo jumla ya shilingi bilioni 2.5 kutoka mapato ya ndani zinatarajiwa kutumika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Aidha, amefafanua kuwa kipaumbele cha halmashauri kwenye bajeti ijayo ni kuendelea na kazi ya kukamilisha vituo vya afya vya Makowo, Kifanya, Luponde na Njombe Mjini vituo ambavyo vipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji, uboreshaji wa huduma za elimu mapambano ya UKIMWI, udumavu/Lishe na utoaji wa mikopo kwa vikundi vya uzalishaji mali.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa baraza kuu la madiwani kujadili rasimu hiyo ya bajeti,mwenyekiti wa halmashauri ya mji Njombe Edwin Mwanzinga alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020,halmashauri imeendelea kufanya vizuri katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Usafi wa Mazingira, Ujenzi, ukusanyaji mapato na yote ni kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Madiwani na Wataalamu katika kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo.
“Katika mwaka wa fedha ujao inabidi tukubaliane kuwa wakati wa kazi ni kazi haitakiwi kuoneana aibu.sisi wanasiasa ndio tunaiangusha Serikali yetu wenyewe kutokana na kauli zetu na kutosimamia ukusanyaji wa mapato ipasavyo kwa hofu ya kutopigiwa kura.Bora kukosa kura lakini tukusanye mapato tukumbuke kuwa wanachi ambao ndio wapiga kura hawatatupigia kura kama maendeleo yasipokuwepo”Amesema Mwanzinga.
Wakichangia kwa nyakati tofauti juu ya makisio ya bajeti hiyo Abuu Mtamike Diwani wa Kata ya Mji Mwema, George Sanga Diwani wa Kata ya Ramadhani, Sigrada Mligo Diwani Viti Maalumu na Ultrick Msema Kata ya Luponde walisema kilio chao kikubwa ni kushuka kwa ukusanyaji wa mapato ya mbao kutokana na mgongano uliopo baina ya TRA Njombe wafanyabiashara wa mbao na Halmashauri juu ya ulipaji wa tozo za mbao na wameomba Mamlaka hizo kukutana na kupata muafaka wa mgogoro huo kwani kwa sasa kunaupotevu wa mapato uliosababishwa na mgogoro huo.
Kwa vipindi tofauti Halmashauri ya Mji Njombe imekuwa ikifanya vizuri katika ukusanyaji mapato kwa kukusanya kwa zaidi ya asilimia 100 na hivyo kuimarisha uwezo wa halmashauri kiuchumi na kuboresha utoaji huduma kwa manufaa ya wananchi wote.