Kansela Merkel kukutana na Rais Erdogan kujadili mkataba wa kuzuwia wakimbizi

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel leo anakutana na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki mjini Istanbul kwa mazungumzo yatakayotuama juu ya hatma ya mkataba wa uhamiaji kati ya Uturuki na Umoja wa Ulaya uliosaidia kupunguza wimbi la wakimbizi barani Ulaya.

Mkataba huo uliopigiwa upatu na Ujerumani, uliutaka Umoja wa Ulaya mwaka 2016 kutoa msaada wa hadi dola bilioni 6.6 kwa Uturuki, kuishawishi serikali mjini Ankara iwazuie wahamiaji kuondoka Ugiriki na kuingia Ulaya.

Mkutano kati ya Merkel na Erdogan unakuja wakati kuna na wasawasi wa kuzuka upya wimbi la wakimbizi kutokana na maelfu ya watu kukimbia mashambulizi mapya ya serikali ya Syria katika jimbo la kaskazini ya nchi hiyo.

Tayari idadi ya wakimbizi wanaoingia Ulaya kutokea Uturuki imeongezeka mwaka uliopita, baada ya watu wanaokimbia machafuko ya Syria na Afghanistan kuwasili Ugiriki na kusababisha msongamano mkubwa katika kambi za kuwahifadhi.
Mpya zaidi Nzee zaidi