Loading...

1/16/2020

Rais Trump atisishia kuweka ushuru kwa magari yanayoingia Marekani kutoka Ulaya

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Annegret Kramp-Karrenbauer amethibitisha taarifa kuwa Marekani imetishia kuongeza ushuru wa asilimia 25 kwa mauzo ya magari kutoka Ulaya.

Ongezeko hilo la ushuru litatekelezwa iwapo Ulaya itaendelea kuunga mkono mpango wa nyuklia wa Iran. Karrenbauer amethibitisha hayo katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa ziara yake jijini London.

Waziri huyo wa Ujerumani ametoa kauli hiyo baada ya gazeti la Washington Post kuripoti kuwa Rais wa Marekani Donald Trump alizitishia Uingereza, Ufaransa na Ujerumani iwapo hazitaukosoa mkataba wa nyuklia uliofikiwa na Iran mnamo mwaka 2015.

China, Marekani na Urusi pia zilitia saini makubaliano hayo lakini baadaye Trump aliiondoa nchi yake na kurejesha vikwazo dhidi ya Iran.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger