Na Thabit madai
Kauli hiyo ameitoa wakati alipofanya ziara yake akiwa na watendaji wa taasisi mbalimbali katika kuangalia uharibifu wa maringira katika fukwe ya bahari eneo la shangani mkabala na hoteli ya africa house.
Mkuu huyo wa Mkoa ametahadharisha kuwa endepo kila sekta zitatatuwa changamoto zilizomo peke yake au kuiyachia taasisi nyengine itatuwe inaweza kupelekea utatuzi wa changamoto hizo kuwa ngumu.
Mkuu wa mkoa amelitaka baraza la manispaa mjini na mamlaka ya bandari zanzibar (zma)pamoja na mamlaka ya mji mkongwe kulifikua shimo liliopo eneo hilo linalotumiwa na wananchi wa maeneo hayo kutupa takataka na kuwataka kuwatengea eneo jengine la kutupa taka.
“hii ni sehemu ya bandari watalii wanatumia kwa ajili ya kupanda boti kwenda visiwani na kupumzika katika ufukwe huu lakini tumepaacha hadi mimefikia hali hii “ alisema mkuu wa mkoa.
Alisema kama maeneo hayo ya vivutio vya utalii yataendelea kuwa katika hali hiyo yataweza kuadhiri sekta hiyo ambayo inamchango mkubwa katika kuingiza mapato ya taifa na kukuza uchumi wa zanzibar.
Mkuu wa Mkoa amelitaka pia Baraza la Manispaa Mjini kuanzia sasa kuweka muda maalumu kwa wananchi kwenda kutupa taka taka majaa badala ya kila mtu kutupa taka kwa wakati wake.
“Zamani watu wakitupa takataka katika majaa wakati maalumu lakini watendaji wameacha kusimamia utaratibu huo sasa kila mtu amekuwa akitupa taka kwa wakati wake”, alisema Mkuu wa Mkoa
Aidha amelitaka Baraza hilo kuwachukuliya hatua za kisheria wafanyabiashara wa vyakula katika maeneo mbalimbali ambao husababisha uharibifu wa mazingira na kuondosha haiba ya mjii Mkongwe.
Naye Mkurungenzi wa Baraza la Manspaa Mjini said Juma Ahmada amemuelezea Mkuu wa Mkoa huyo kuwa tayari wamepiga marufuku eneo hilo kutupa taka lakini wakazi wa maeneo hayo hawakuweza kutii angizo la manispaa na badala yake hutumia nyakati za usiku kutupa taka hizo.
Amewataka wananchi kufahamu kuwa Baraza lake limeanza kutumia sheria ya faini ya papo kwa papo kwa makosa mbalimbali likiwemo kosa la uharibifu wa mazingira.
Kwa upande wake afisa wa Mamlaka ya usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA) Abedi Isimail Aboubakar Alisema sehemu kubwa ya ukuta unaozuia bahari eneo la Shangani limeathirika.
Ameshauri taasisi zote husika kukaapamoja na kuangalia namna eneo hilo litakavyo weza kufanyiwa matengenezo kama yaliyofanywa eneo la forodhani hali iliyopelekea kuwa ni kuvutio kikubwa cha watalii wa ndani na nje.
