Waziri Ummy: Tanzania haijakumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa virusi Cha Corona


Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, imewatahadharisha wananchi kujilinda na tishio mpya la ugonjwa mpya unaosababishwa na kirusi Cha Corona(Novel Corona Virus 2019- nCoV) ambao umelikumba taifa la China na kuwepo kwa taarifa kusambaa katika Mataifa Mengine.


Akizungumza na Wanahabari leo Bungeni Jijini Dodoma, Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu, kuhusu ugonjwa huo, amesema ingawa kwa hapa nchini hakuna mgonjwa wala mtu anayehisiwa kuwa na ugonjwa huo, lakini amewataka wananchi kuchukua hatua ya kujilinda na kirusi hicho hatari.


"Wizara ya Afya inaendelea kutoa tahadhari kwa umma kuhusu Maendeleo ya mlipuko wa ugonjwa wa homa Kali ya Mapafu inayosababishwa na kirusi aina ya Corona ulioikumba nchi ya China na nyingine na umekuwa ukisambaa kwa kasi sana ambapo kumekuwa na ongezeko la wagonjwa pamoja na vifo katika kipindi kifupi" amesema Waziri Ummy.


Amesema kwa mujibu wa Shirika  la Afya Duniani (WHO) tangu mlipuko wa ugonjwa huo uanze katika Mji wa Wuhan uliopo katika jimbo Hubel Nchini China mwezi Disemba, 2019 hadi 28, Januari 2020 na jumla ya watu 4593 wamethibitishwa na 4537 na vifo 106 kutoka China.


Aidha ameongeza kuwa "Ugonjwa huu umesambaa na Mataifa mengine 14 Duniani zikiwemo Japani, Jamhuri ya Korea, Vietnam, Sangapore, Australia, Malaysia,Nepal, Sri Lanka, Marekani, Canada, Ufaransa  Ujerumani

Cambodia na Thailand," amesema.


Amesema Ugonjwa huo husababishwa na kirusi Cha Corona ambacho ni tofauti na virusi vingine vya Jamii hiyo ambavyo viliwahi kusababisha na kusababisha milipuko ya Magonjwa kama "SARS-CoV" na MERS-CoV  Corona Virusi mwaka 2013.


Amesema kuwa "Dalili za ugonjwa huu ni pamoja Homa, mafua kuumwa kichwa, Mwili kuchoka, kikohoz, kubanwa mbavu, maumivu ya misuli, vidonda vya Koo, Mapafu kuathirika, kupumua kwa shida na hata kifo, ugonjwa huo hauna chanjo Wala tiba ya moja kwa moja" amesema.


Aidha amesema Kama Wizara wanafanya kila jitihada kuhakikisha wanazuia ugonjwa huo kuingia hapa nchini, kwa kufanya jitihada mbalimbali pia wanafanya maandalizi endapo ugonjwa huo utaingia namna ya kuukabili kwa kutenga maeneo maalumu.


Pia amewatahadharisha watu wanaotarajia kusafiri kwenda Mataifa hayo ambako ugonjwa huo upo au wanahisiwa kuwa na mlipuko huo, huku akibainisha hakuna mtanzania ambaye anaishi nchini China kaathirika na ugonjwa huo wote wapo salama mpaka Sasa.
Mpya zaidi Nzee zaidi