Breaking News: Man City yafungiwa na UEFA

Umoja wa vyama vya soka Ulaya (UEFA) leo umetangaza kuifungia club ya Man City ya England kwa misimu miwili mfululizo kwa kutenda makosa mawili.

Kwa mujibu wa UEFA ni kuwa Man City imefungiwa (2020/21 & 2021/22) kushiriki michuano ya Ulaya ngazi ya club na faini ya pound milioni 24.9 (Tsh bilioni 74.9) kwa kosa la kuvunja sheria za UEFA za leseni ya vilabu na Financial Fair Play.

Hata hivyo kosa jingine lililosababisha adhabu hiyo ni kuwa Man City hawakutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi, Financial Fair Play kwa mujibu wa UEFA ni kuwa sheria inataka vilabu vifanye usajili kulingana na pesa inazozalisha na sio kuliko kiasi inachoingiza.