CHAURU wakamata mzani feki



Na Omary Mngindo, Bagamoyo.

Chama cha Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) kinachofanya shughuli zake za kilimo Kitongoji cha CHAURU, Kijiji cha Visezi Kata ya Vigwaza Bagamoyo Pwani, kimekamata mzani "feki" uliokuwa unawaibia wakulima kilo 14 kwenye kila gunia la kilo mia.

Mzani huo unaodaiwa ulikuwa unatumiwa na baadhi ya wanachama wasiowaaminifu kwenyw kitengo cha mashine, kwa muda mrefu walikiwa wanautumia kwa kupima magunia ya mpunga wa wanachama waliokuwa aanakoboa mpunga, ambapo kwenye kila gunia wahusika walikiwa wanapata faida ya haramu kilo 14.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa ushirika Sadala Chacha mbele ya Wanachama-CHAURU hao kwenye mkutano Mkuu wa mwaka uliofanyika ndani ya mashamba hayo, ambapo alisema kuwa alipewa taarifa na mmoja wa wanachama ambae kwa sasa yupo nje ya Mkoa wa Pwani.

"Nilipigiwa simu na mmoja wa watu waliokuwa wanajihusisha na upimaji mpunga kwenye kwamba kuna mzani unatumika ambao umezidiahwa uzito, kila kunapokobolewa mpunga wanapata hasara ya kilo 14 kwa maana mpimaji wanapata faida haramu ya kilo hizo," alisema Chacha.

Aliongeza kwamba kwa sasa mhusika huyo amekamatwa wakati uchunguzi unaendelea, na kwamba ikibainika kweli alikuwa anajihusisha na jambo hilo atafikishwa katika vyombo husika ili hatua za kisheria ziweze kichukuliwa.

"Mtuhumiwa huyo anaendelea kuchunguzwa ikibainika alihusika na hujuma hiyo kwa wanachama atafikishwa kwenye vyombo vinavyohusiam ili hatu zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa, tushirikane katika kuwadhibiti wataohusika na hujuma," alisema Chacha.

Katika mkutano huo wana-CHAURU walijadili masuala mbalimbi ya kimaendeleo ikiwemo kulipia madeni wanayodaiwa na ushirika huo, ambapo mwisho wa ulipwaji huo ni mwezi Novemba mwaka huu.

Mmoja wa wanachama wa CHAURU akichangia mada alianza kwa kuupongeza uongozi huo kwa namna unavyowajibika, huku akiwataka wawe makini katika kazi zao na kutoyumba kwenye masuala ya kikazi.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items