Jeshi la Marekani limeimarisha wito wake kwa Korea kusini kulipia zaidi gharama za ulinzi na kuonya kuhusu athari zitakazokuwepo iwapo mkataba hautaafikiwa hivi karibuni.
Haya yanajiri huku waziri wa ulinzi wa Korea Kusini Kyeong-doo Jeong akitarajiwa kukutana na mwenzake wa Marekani Mars Esper siku ya Jumatatu mjini Washington.
Kyeong-doo na Mark Esper, wanatarajiwa kuzungumzia kuhusu mkwamo na Korea Kaskazini pamoja na mipango ya kuipa Korea Kusini udhibiti wa vikosi vya kijeshi katika rasi hiyo ya Korea wakati wa vita.
Lakini kinachoongoza katika masuala hayo yote, ni mazungumzo kuhusu kiasi cha pesa ambacho Korea Kusini inapaswa kulipa katika kudumisha takriban vikosi 28500 vya Marekani katika eneo hilo.
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Korea Kusini, alikataa kuzungumzia kuhusu mazungumzo hayo lakini akasema kuwa nchi hiyo inaimarisha juhudi za kuafikia mkataba mapema iwezekanavyo kupunguza matatizo yoyote.