Virusi vya Corona: Vikao vya bunge la China vyahairishwa kwa mara ya kwanza tangu mapinduzi ya utamaduni

Kikao cha bunge la China kilichokuwa kianze March 5 kimehairishwa kutokana na hofu ya virusi vipya vya Corona (Kovid-19).

Uamuzi huo umefanywa na baraza la uongozi wa bunge katika kikao chake cha leo.

Kikao hicho ambacho kwa uchache hudumu kwa muda wa siku 10, hujumuisha wajumbe elfu 5000 kutoka maeneo mbalimbali na hukutana jijini Beijing.

Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano wa bunge kuhairishwa tangu mapinduzi ya utamaduni  (1966-1976)
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items