China kulipa Yuan elfu 10 kwa kila mgonjwa wa Corona atakayejisalimisha kwenye vituo vya afya

Nchini China yeyote mwenye dalili ya kuambukizwa virusi vya Corona (Covid-19) akatoa taarifa kisha kupimwa na kugundulika na virusi hivyo atalipwa Yuan elfu 10, sawa na dola takriban elfu 1 na mia 5.

Hatua hiyo imechukuliwa na mamlaka ya jimbo la Hubey, katika mji wa Qianjiang katika kujaribu kudhibiti kusambaa kwa mlipuko wa maambukizi.

Mamlaka zimetaka watu wapewe motisha ili waweze kutoa taarifa juu dalili za kuambukizwa, Kwa yeyote atakayejisalimisha mwenyewe atalipwa kiasi cha Yuan elfu 10 takribani dola elfu 1 na mia tano.

Pesa hiyo itatolewa kwa wale tu ambao matokeo yao yatagundulika kuwa chanya, yaani wana maambukizi. Kwa wale ambao watahisi kuwa wameambukizwa na matokeo ya vipimo yakaonyesha hawajaambukizwa watalipwa yuan elfu 1, na kwa wale ambao kuna hakuna uhakika kama wameambukizwa au la watapewa yuan elfu 2.