Na Ahmad Mmow, Lindi.
Mkuu wà wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai ametoa wito kwa wahisani wa ndani na nje ya nchi ambao wameguswa na madhara waliyopata waathirika wà mafuriko wilayani humo wasisite kupeleka misaada. Kwani bado inahitajika sana.
Ngubiagai ameyasema hayo alipozungumza na Katibu mkuu wà taasisi ya kuendeleza na kudumisha urafiki baina ya wananchi wa Tanzania na China, Joseph Kahama mjini Kilwa Masoko baada ya kupokea msaada na kufanya mazungumzo na katibu mkuu huyo wa taasisi.
Ngubiagai ambae katika mazungumzo hayo aliishukuru kampuni ya ujenzi ya CCECC ya China kwa kukubali kusaidia kukarabati baadhi ya miundombinu iliyoharibika kutokana na mafuriko hayo, alisema mafuriko hayo yamesababisha madhara makubwa kwa watu na miundombinu mbalimbali. Kwahiyo bado kunahaja yakuendelea kupelekwa misaada wilayani humo.
Alisema mafuriko hayo yamesababisha kufuta shule ya msingi ya Njinjo. Baada ya miundo mbinu yake kuharibiwa vibaya na maji yaliyosababishwa na mafuriko hayo makubwa kuwahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.
"Kwahiyo naendelea kutoa wito kwa wadau muendelee kusaidia. Bado kuna mahitaji makubwa ya kukarabati miundombinu, chakula, dawa na hata mbegu kwa wananchi wetu hawa," alisisitiza Ngubiagai.
Kwa upande wake, Kahama alisema wameguswa na matatizo yaliyowakuta wananchi wa mkoa wa Lindi, kwani wanatambua mafuriko yaliyoukumba mkoa wa huo yamesababisha madhara mbalimbali. Ikiwemo wananchi kukosa makazi,na wengine kupata maradhi .
Alisema kutokana na madhara hayo wameamua kutoa msaada wa madawa mbalimbali ya binadamu na madaktari bigwa kutoka nchini China. Ambao wamekubali kuja kutoa huduma za afya kwa waathirika wa mafuriko hayo.
