Kansela Merkel aanza ziara yake Afrika Kusini

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajiwa kuwasili Afrika Kusini leo kujadili masuala ya biashara, uwekezaji na nishati na nchi hiyo ambayo ni mshirika wake mkubwa wa kibiashara barani Afrika.

Merkel na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa pia wanatarajiwa kujadili ushirikiano katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo nchi hizo mbili zinahudumu kwa kipindi cha miaka miwili kama wanachama wasio wa kudumu.

Ofisi ya Ramaphosa imesema Ujerumani na Afrika Kusini zimedhamiria kuhimiza amani ya ulimwengu na usalama, kuimarisha na kuzifanyia mageuzi taasisi za kimataifa na kulishughulikia suala la mabadiliko ya tabia nchi.

Afrika Kusini itachukua uwenyekiti wa Umoja wa Afrika, ikiwa ni fursa ya kuonyesha uongozi katika masuala ya siasa za kikanda wakati wa muhula wake wa mwaka mmoja.
Mpya zaidi Nzee zaidi