https://monetag.com/?ref_id=TTIb Padre aliyewasaidia watu 'alinyanyasa kingono wanawake sita' | Muungwana BLOG

Padre aliyewasaidia watu 'alinyanyasa kingono wanawake sita'

Kiongozi wa kidini mwanzilishi wa shirika la wenye matatizo ya kusoma alinyanyasa wanawake sita nchini Ufaransa, kwa mujibu wa ripoti ya ndani.

Padri Jean Vanier raia wa Canada ni mwanzilishi wa shirika kubwa la kimataifa duniani la L'Arche nchini Ufaransa mwaka 1964, ambaye alifariki mwaka jana akiwa na umri wa miaka 90.

Miongoni mwa aliowanyanyasa hakuna hata mmoja ambaye ni mlemavu, ripoti hiyo inasema.

Uchunguzi dhidi ya Vanier ulipendekezwa mwaka jana na shirika aliloanzisha mwenyewe baada ya kuzuka kwa tuhuma hizo.

Ripoti kamili inatarajiwa kuchapishwa siku chache zijazo.

"Tumeshutuka kwa taaifa hizi na tuna laani vitendo hivyo, ambavyo vinakinzana na maadili ambayo Jean Vanier alidai kuwa nayo, na hayaendani kabisa na heshima na maadili ya mtu, tofauti kabisa na misingi ya shirika la L'Arche," hayo yameandikwa katika tovuti ya shirika la kimataifa la L'Arche.

Shirika hilo linaendesha makazi na vituo ambapo watu ama walio au wasio na ulemavu huishi kwa pamoja na linaendesha shughuli zake katika nchi 38 kote duniani lenye wanachama karibia 10,000.