VIDEO: Halima Mdee agoma kumpa mkono mashinji Mahakamani


ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dkt Vincent Mashinji, amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu, Februari 24, 2020, na kukutana na viongozi wa Chadema kwa ajili ya kusikiliza kesi inayowakabili.

Mashinji aliyehamia CCM na viongozi wengine wanane wa chama hicho wanakabiliwa na kesi ya jinai yenye mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi.

Baada ya kuingia mahakamani alianza kuwasalimia waliokuwa viongozi wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe, Peter Msigwa, Esther Bulaya na wengine waliokuwepo mahakamani hapo.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI........USISAHAU KUSUBSCRIBE

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items