VIDEO: Kwa uchungu hukumu ya kabendera, amlilia mama yake baada ya kuachiwa


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imemuhukumu Mwandishi wa Habari za uchunguzi Erick Kabendera kulipa faini na fidia ya jumla ya Tsh. Milioni 273 baada ya kukiri makosa yaliyokuwa yakimkabili ya utakatishaji fedha na ukwepaji kodi huku akiondolewa shitaka la kuongoza genge la uhalifu.

Mahakama imetoa uamuzi huo leo Jumatatu, Februari 24, 2020, baada ya mwenendo wa kesi iliyokuwa ikimkabili inafuatia kukamilika kwa mazungumzo na makubaliano baina yake na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP).

Kabendera amekiri shtaka la kukwepa kodi ya TZS milioni 173. Ameahidi kulipa kiasi hicho kwa mafungu ndani ya kipindi cha miezi 6. Kwa shtaka hilo, mahakama imeamuru alipe faini TZS 250,000 au kifungo cha miezi sita jela.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items