Virusi vya Corona: Maambukizi mapya yapungua China

Maambukizi mapya ya virusi vya Corona nchini China yameendelea kushuka leo, ambapo watu 1,749 zaidi wameambukizwa na vifo zaidi 136 wakati afisa wa ngazi ya juu ktika eneo kulikoanzia mripuko huo ameapa kumpata na kumtenga kila mtu aliyeathirika katika mji huo ifikapo jioni leo.

 Leo Jumatano itakuwa siku ya mwisho ya kampeni ya nyumba hadi nyumba mjini Wuhan, mji ulioko katikati ya China ambako virusi hivyo vilianzia, kumuondoa mtu yeyote ambaye ana dalili ambazo maafisa wameshindwa kuziona hadi sasa.

China bara imeripoti jumla ya watu 74,185 za maambukizi ya virusi hivyo vya Corona na vifo 2,004.

Maambukizi mapya yamepungua na kufikia watu 2,000 katika muda wa siku mbili zilizopita, lakini maafisa na wachambuzi wameaonya kuwa kitisho za virusi hivyo bado kipo wakati wafanyakazi wanaanza taratibu kurejea kazini kufuatia sikukuu iliyorefushwa ya mwaka mpya wa China.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items