Waandamanaji Iraq waapa kuendeleza maandamano

Waandamanaji wanaoipinga serikali nchini Iraq wameapa leo kuendelea na wimbi la maandamano mnamo wakati wakiwazika wenzao saba waliouawa usiku wa kuamkia leo wakati wa vurugu zinazodaiwa kufanywa na wafuasi wa kiongozi wa kidini mwenye ushawishi mkubwa.

Wafuasi wa kiongozi wa Kiislamu wa dhehebu ya Moqtada Sadr, ambaye ni mwanamgambo aliyegeukia siasa, walivamia kambi ya waandamanaji katika mji wa Najaf usiku wa kuamkia leo.

 Vurugu za usiku wa kuamkia leo mjini humo ni mbaya zaidi katika machafuko hayo kati ya upande wa waandamanaji na wafuasi wa Sadr ambaye awali aliyaunga mkono maandamano hayo lakini mwishoni mwa wiki iliyopita, kwa ghafla alijitenga na vuguvugu hilo.

Sadr alimuidhinisha Mohammad Allawi kuwa waziri mkuu mpya mteule, hali ambayo inakinzana na msimamo wa waandamanaji wanaomkataa mwanasiasa huyo kuwa ni mtu wa mfumo wa sasa.
Mpya zaidi Nzee zaidi