Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona Uganda, Rwanda yaongezeka kwa kasi


Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona (Covid-19) katika nchi za Afrika Mashariki za Uganda na Rwanda imepaa kwa kasi huku nchi hizo zikipambana kuzuia maambukizi zaidi.

Nchini Uganda jana usiku wametangaza wagonjwa wapya nane na kufikisha idadi ya wagonjwa wa Covid-19 kufikia tisa.

Wagonjwa hao wapya wanane wote ni raia wa Uganda ambao wamerejea nchini humo kutokea Dubai baina ya tarehe 20 na 22 mwezi huu.

Waziri wa Afya wa Uganda, Jane Ruth Aceng amewaambia wanahabari kuwa kufikia sasa nchi hiyo imebaini wasafiri 2,661 wakiwemo raia wa nchi hiyo ambao wanaweza kuwa na hatari ya kusambaza maambukizi na watu wote hao wapo chini ya uangalizi maaalumu.
azia raia wake kuchukua tahadhari kujilinda na maambukizi hususani kwenye maeneo yenye mikusanyiko
"Kati ya hao, watu 1,356 wanafuatiliwa kwa ukaribu; watu 774 wapo karantini kwenye maeneo maalumu yaliyotengwa huku 582 wakijitenga wenyewe kwa kujiweka karantini," ameeleza waziri Aceng.


Wagonjwa wapya wa virusi vya corona 17 wametangazwa jana usiku nchini Rwanda na kufanya idadi ya maambukizi nchini humo kufikia watu 36.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya ya Rwanda mchanganuo wa wagonjwa hao 17 ni; wasafiri tisa walioingia Rwanda kutoka Dubai, wasafiri watatu kutoka Kenya, wawili kutoka Marekani, mmoja kutoka India na mmoja kutoka Qatar.

Rwanda imepiga marufuku raia wake kutoka nje isipokuwa kwenda kununua chakula na dawa
Mtu mmoja pia amekutwa na virusi hivyo baada ya kutangamana na mtu ambaye aligundulika navyo hapo awali.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo, wasafiri wote hao waliingia nchini Rwanda baina ya tarehe 17 na 20.

Wagonjwa wote 36 kwa mujibu wa Wizara ya Afya wa Rwanda wanaendelea na matibabu na wapo katika hali nzuri.